TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 01.11.2021 : VAN DE BEEK, CONTE, POGBA, HERNANDEZ, CEBALLOS, GOUIRI
Real Madrid wanamuangalia kwa karibu kiungo wa kati mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, pamoja na kiungo wa kati wa safu ya nyuma wa Chelsea na Ujerumani Rudiger, wenye umri wa miaka 28, kama wachezaji wapya wanaoweza kusaini nao mkataba katika klabu hiyo. (Marca)
Barcelona wana nia ya kumchukua kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 24, kwa mkopo (Sport - in Spanish)
Tottenham wanafanya juhudi kufanya mkataba ambao utamwenzesha Antonio Conte kuchukua nafasia ya Nuno Espirito Santokama meneja. (Tuttomercato - in Italian)
Meneja wa Porto Sergio Conceicao, 46, anafuatiliwa kama mtu anayeeza kuchukua nafasi ya Nuno kama meneja wa Tottenham . (Standard)
Ryan Mason, 30, atawekwa kama kiongozi wa muda wa Tottenham hadi Krismasi. (Football Insider)
Paris St-Germain pia wanaifuatilia kwa karibu hali ya Pogba katika Manchester United. (Le10 Sport - in French)
Kiungo wa safu ya nyuma-kushoto wa Ufaransa Theo Hernandez, 24, amejipanga kkuhama Manchester City huju akipendelea kusaini mkataba mpya katika AC Milan. (Calciomercato - in Italian)
Manchester United walikosa fursa ya kusiani mkataba na kiungo wa kati wa PSG na Senegal Idrissa Gueye, 32, msimu uliopita kwasababu hawakuweza kuwa tayari kutoa ofa kwa wachezaji kadhaa waliopo katika klabu hiyo. (Mail)elezea
Arsenal bado wanamfuatilia kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Dani Ceballos, 25, licha ya kwamba mkataba wake wa mkopo unatarajia kumalizika baada ya miaka miwili . (El Nacional, via TEAMtalk)
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 01.11.2021 : Van de Beek, Conte, Pogba, Hernandez, Ceballos, Gouiri
Mshambuliaji wa Nice na ufaransa wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21, Amine Gouiri, 21 analengwa na Manchester City. (Fichajes - in Spanish)
Mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic anataka kujiunga na Juventus. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21-pia amehusishwa na Manchester City. (Tuttosport - in Italian)
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: