PABLO AANZA NA TATIZO LA CHAI KWA WACHEZAJI, ATOA MASHARITI MAGUMU BALAA

CHUKUA hii. Simba ndiyo timu pekee kwenye Ligi ya Tanzania yenye Kocha Mhispania aliyewahi kufundisha kwenye Laliga. Ile unayoiona kwenye Kibandaumiza. Kocha huyo, Pablo Franco ameanza kazi. Siku ya kwanza alisalimiana na wachezaji gym na benchi la ufundi.

Akiwa gym mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, alisalimia kila mchezaji na kumwambia anafurahia kumuona. Lakini juzi asubuhi baada ya mazoezini akaanza na masharti kwenye chai baada ya kushtukia kwamba kuna jambo haliendi sawa na linaweza kumharibia utaratibu mbele ya safari.

Pablo ambaye rekodi zake zinaonyesha amefundisha Real Madrid na Getafe aliwaambia wachezaji wote kwamba; “Nataka muda wa chai wote tuwe mezani kwa pamoja hakuna mtu kubaki nyuma wala vyumbani.”

Kocha huyo alilazimika kutoa muongozo huo baada ya kushuhudia kwamba kuna baadhi ya mambo yalikuwa yakilega na kila mmoja akija mezani kwa muda anaotaka yeye jambo ambalo kiutaratibu wa kazi halileti mtiririko mzuri wa kinidhamu.

KINA MANULA
Lakini Pablo amewaambia viongozi kwamba ataendelea kuweka utaratibu wake wa kazi taratibu na sasa anasubiri kina Aishi Manula, Muzamiru Yassin, Kennedy Juma, Tshabalala, Kapombe,Nyoni, Bocco na mastaa wengine walioko timu za Taifa warejee ndipo afanye kikao cha pamoja na wachezaji wote.

Aliwaambia kwamba hawezi kutoa maelekezo marambili ndio maana anataka kuzungumza nao kwa pamoja kila mmoja asikie kutoka kwake mikakati na wao awasikilize ili kupanga mikakati ya pamoja.

Lakini ataendelea na programu na kikosi kilichopo kujiandaa na mechi zijazo za Ligi.


MAZOEZINI
Kwa mara ya kwanza alikiongoza kikosi hicho katika mazoezi aina mbalimbali Alhamisi asubuhi yaliyofanyika katika Uwanja wa Isamuyo, Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo yaliyoanza saa 2:30, wachezaji walikimbia pole pole kwa kuzunguka uwanja, baadae waliingia katika mazoezi ya viungo.

Katika mazoezi hayo ya viungo aina mbalimbali waliwekewa na koni ndefu na fupi kwani muda mwingine wachezaji walitakiwa kuziruka.

Kwenye awamu hizi mbili za mazoezi ya mwisho yalikuwa yakisimamiwa na wasaidizi wawili, Hitimana Thiery na Selemani Matola huku Franco akiwa amesimama pembeni kusoma mambo mbalimbali.

Baada ya kumaliza aina hizo mbili za mazoezi Franco aliingia katikati ya uwanja katika eneo la kuchezea kisha kuwapa mazoezi mbalimbali ya kucheza mpira ikiwemo kushambulia na kukaba.

Franco katika mazoezi hayo ya kucheza alitaka kila mchezaji kutogusa mpira zaidi ya mara mbili na kupiga pasi ya haraka na uhakika kwa mwenzake na kama ikitokea ameupoteza anatakiwa kukaba kwa haraka ili kuutuafuta mpira mpaka kuupata.

Katika kuhakikisha zoezi hilo la kucheza kwa kila mchezaji kutokaa na mpira kwa muda mrefu, kugusa mpira si zaidi ya mara mbili, kupiga pasi za uhakika, kushambulia na kuutafuta mpira kwa haraka ukipotea walimaliza mazoezi kwa kucheza mechi.

Mechi hiyo ilikuwa nusu ya uwanja na walicheza wenyewe kwa wenyewe upande mmoja ulikuwa na makipa, Benno Kakolanya na Ally Salim huku kwingine alikuwepo, Jeremia Kisubi. Mechi mazoezi ilikuwa ya kuvutia kwani kila mchezaji alikuwa na hamu ya kucheza wakati timu iliyokuwa imevaa bipsi ilifungwa mabao 2-1, ambayo yalifungwa na Ibrahim Ajibu na Hassan Dilunga wakati wale ambao hawakuwa na bipsi bao lao lilifungwa na Bernard Morrison.

Kocha msaidizi, Hitimana alisema wanaendelea vizuri na mazoezi kwa waliopo

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.