MAPYA YAIBUKA UFUNDI NA UTAALAMU WA PABLO SIMBA
KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco juzi jioni alitesti mitambo kwa vijana wake ikiwa ni mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo, huku akiwapa madini kwa kutumia chati akiwataka kupiga pira biriani kuwapa raha mashabiki wao.
Kocha huyo alionekana akiyafanya hayo kwa vijana wake wakati wa pambano la kirafiki baina ya Simba na Kituo cha Kukuza vipaji cha Cambiaso, uliochezwa Uwanja wa Boko Veterani na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, huku Mhispania huyo akionekana kuwahimiza vijana wake kupiga pira tamu.
Katika mchezo huo mkali na uliokuwa wa kwanza kwa Pablo kama kocha wa Simba, alikuwa akiwaelekeza zaidi wachezaji wake wote wacheze soka la chini la utulivu bila ya papara sambamba na kupiga pasi nyingi kuelekea mbele langoni mwa wapinzani wao.
Pablo alitumia mfumo wa 4-3-3 katika mchezo huo na aliwataka mabeki wake wa pembeni na mawinga wawe wepesi kufanya hivyo. Mfumo wa kutuimia mabeki kama mawinga ulikuwa pia ukitumiwa na watangulizi wake, Sven Vanderbroeck na Didier Gomes aliyetimuliwa hivi karibuni.
Pablo mara kwa mara alisikika akimhimiza beki wa kushoto Gadiel Michael awe mwepesi kuachia krosi na sio kukaa na mpira sana.
Pablo akisaidiana Seleman Matola na Thiery Hitimana walionekana kuwa makini muda wote wakihakikisha wachezaji wanafanya kile wanachokielekeza na kuwapa burudani mashabiki waliohudhuria mchezo huo.ADVERTISEMENT
Wachezaji wote kuanzia kipa alikuwa hatakiwi kubutua badala yake alitakiwa kujiamini na akipokea mpira basi atoe haraka kwa mabeki wake.
Kipa Beno Kakolanya aliyecheza kwa dakika 4 alionekana akiendana na falsafa hiyo baada ya kucheza vizuri na mabeki wake, bila kuruhusu bao hadi kipindi cha pili alipoingia Jeremiah Kisubi aliyeruhusu nyavu zake ziguswe mara mbili.
Mabeki wa kati waliocheza juzi Pascal Wawa na Abdulswamad Kassim walikuwa wanacheza kwa kutumia nguvu na akili na muda wote walisisitizwa wasibutue.
Eneo la kiungo Jonas Mkude, Hassan Dilunga na Ibrahim Ajibu walicheza kwa maelewano ya juu, huku chiniwakimuacha Mkude na wao walikuwa wepesi katika kupeleka mashambulizi mbele.
Ajibu na Dilunga walitakiwa muda wote hesabu zao ziwe kusonga mbele kwa pasi zenye macho na zinazofika kwa ufasaha.
Upande wa ushambuliaji Pablo aliwaweka Yusuph Mhilu, Jimson Mwanuke na Josephat Mbaga na muda wote waliipa wakati mgumu safu ya ulinzi ya Cambiaso.
Mbaga, alikuwa amesimama eneo la kati, huku Mwanuke na Mhilu wakitumia spidi zao kupenya mabeki na jambo hilo lilionyesha kumfurahisha kocha huyo.
Pablo alionekana kuwataka washambuliaji wawe wepesi kupenya na kupiga mashuti nje ya boksi, pia kuingia ndani ya boksi.
Wachezaji walioanza mchezo huo ni Beno Kakolanya/Jeremiah Kisubi, Yusuph, Gadiel Michael, Pascal Wawa na Abdulsamad Kassim.
Wengine ni Jonas Mkude, Yusuph Mhilu, Hassan Dilunga, Josephat Mbaga, Jimson Mwanuke na Ibrahim Ajibu.
UNAHODHA MOTO
Katika mchezo huo nahodha alikuwa Gadiel Michael aliyeongoza hadi dakika 76 na kutolewa.
Wakati anatoka Gadiel aliangalia uwanjani na kutaka kumpa Ajibu kitambaa, lakini alipoitwa alikidaka n kukiepeleka kwa Dilunga, ambaye naye alikikataa na kukipeleka nje katika benchi la ufundi na kuendelea kucheza
Ajibu na Gadiel kwavipindi tofauti waliwahi kuwa manahodha walipokuwa Yanga.
MSIKIE HITIMANA
Kocha msaidizi wa Simba, Thiery Hitimana alisema mechi hiyo ilikuwa maalum kwa kocha Pablo kuwaona wachezaji wake.
Hitimana alisema, Pablo hajakaa na wachezaji na hajui uwezo wao ndio maana aliomba mechi hiyo na sasa anasubiri wale waliokuwa na timu za taifa kuendelea na programu zake kujianda na mechi za Ligi na zile za CAF.
Akizungumzia kukosekana kwa Benard Morrison na Pape Sakho alisema;
”Morrison ameenda kwao Ghana kwa lengo la kubadili hati yake ya kusafiria, huku Sakho akiwa bado hajapona vizuri kuanza mikikimikiki uwanjani kama ya mechi.”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: