MANARA TENAAH...ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU 'KAMATI KAMATI' ZA MSHINDO MSOLA..AMTAJA SENZO...


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amewashukuru Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msola kwa kuunda kamati ya Utendaji ambayo inaisapoti timu hiyo kuhakikisha inafanya vizuri.

Manara amesema kamati hiyo pamoja na kaimu Mtendaji mkuu wao, Senzo Mazingisa wamekuwa wakiwasapoti kwa hali na mali.

“Kamati ya mwenyekiti wetu pamoja na mtendaji mkuu wamekuwa bega kwa bega kuhakikisha timu inashinda na kweli imekuwa hivyo,” amesema Manara.

Msemaji huyo pia aliwashukuru wafadhili wa klabu hiyo baada ya kuhakikisha timu yao inazidi kuwa imara katika kila idara.

“Wakati Yanga ikiwa inafanya vizuri tujue kabisa kuna wafadhili wetu wakubwa na wengine kwa pamoja wanaiunga mkono kuifanya timu kuwa hivi mnayoiona.”

Manara ameongeza akisema; ”Lazima niwashukuru hawa watu kwasababu wana umuhimu wao”.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.