KUELEKEA MECHI YA LEO, RUVU YAITISHIA YANGA, YASEMA HAYA

Dar es Salaam. Yanga ina nafasi ya kuweka rekodi mpya ya kuibuka na ushindi bila kuruhusu bao katika mechi tano mfululizo za mwanzo za Ligi Kuu ikiwa itaifunga Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Lakini Ruvu Shooting imejinasibu kuwa timu ya kwanza kuanza kuifunga Yanga msimu huu katika ligi, kwa mujibu wa kocha msaidizi wa timu hiyo, Rajab Nakuchema.

Lakini kama Yanga itashinda, itapiga ndege wawili kwa jiwe moja kwani itanufaika zaidi kwa kuongeza pengo la pointi baina yake na washindani wake wakuu katika mbio za ubingwa, Simba na Azam.

Ushindi katika mchezo wa leo, utaifanya Yanga ifikishe pointi 15, ambazo zitaitangulia Simba inayotetea ubingwa kwa tofauti ya pointi saba na itawaacha Azam FC kwa pointi 11, jambo ambalo

litawaweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

Yanga imekuwa na rekodi ya ubabe inapokutana na Ruvu Shooting kwenye Ligi Kuu na mara kwa mara imekuwa ikipata ya ushindi.

Hilo linadhihirishwa na mechi 10 zilizopita ambazo zilikutanisha timu hizo kwenye ligi na Yanga imeibuka na ushindi mara nane, kutoka sare moja huku ikipoteza mchezo mmojapekee.

Ni mechi ambayo inategemewa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uzoefu wa kocha wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa katika Ligi Kuu na mechi dhidi ya timu za Yanga, Azam na Simba na mara kwa mara zimekuwa zikitoa upinzani kwa vigogo.

Wakati Yanga ikiingia katika mchezo huo ikiwa na matokeo bora ya kupata ushindi mara nne, Ruvu Shooting yenyewe imepata ushindi mara mbili na kupoteza miwili.

Mbali na mechi hiyo, katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Azam FC itaikaribisha Geita Gold ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.