KISA MAZOEZI YA YANGA..AUCHO ASHINDWA KUJIZUIA...AWACHANA WACHEZAJI WENZAKE..NABI ASHANGAA TU...

YANGA juzi usiku ilikuwa uwanjani ikipambana na Azam FC katika mchezo wa nne wa Ligi Kuu Bara na kikosi chao kuna mastaa wapya saba waliokiongeza ubora, lakini kiungo wao mmoja, Khalid Aucho amemsapraizi kocha Nasreddine Nabi na mastaa wenzake mazoezini kuonyesha asivyo na masihara.

Kiungo kutoka Uganda, alifanya kitu ambacho sio rahisi kwa wachezaji na hata manahodha ni wachache wanaomudu katika ratiba ya mazoezi baada ya kuwataka wenzake wasibweteke.

Aucho aliwashtukia wenzake kuwa hawajitumi mazoezini kama watu walioridhika na mafanikio ya muda mfupi na kuwaambia hapana, akasimamisha ratiba hiyo akiwataka kila mmoja wao kujituma.

Aliyefichua hilo ni Kocha Nabi, aliyesema kiungo huyo alimshtua akitaka kila mmoja kupambana mazoezini.

Nabi alisema Aucho aliwataka wenzake kuacha kubweteka na kushinda mechi tatu (kabla ya jana) na ligi bado ngumu vinginevyo watapoteza malengo.

“Nilishtuka alipowatamkia vile wenzake tukiwa mazoezini. Ni mmoja kati ya wachezaji waliokomaa kiakili tulionao ambao wanatambua umuhimu wa kushindana kuanzia mazoezini,” alifafanua Nabi na kuongeza.

“Alieleweka kwa wenzake, kwani kila mmoja alibadilika na kuongeza juhudi unahitaji kuwa na watu bora kama hao kwenye timu na hii ni kielelezo kingine kwamba tuna timu imara.”

Nabi alisema anafurahia ukomavu wa Aucho katika kikosi chao ambapo endapo kila mchezaji wake atajitambua kwa kiwango hicho msimu huu wanaweza kufikia malengo.

“Sina mashaka na akili ya wachezaji wangu, ila unahitaji kuwa na watu wanaotambua kwanini wako hapa Yanga na uzito wa kujituma kwa ajili ya klabu kubwa kama hii. Tuna deni kubwa hapa msimu huu kuhakikisha mashabiki wote wanafurahia haya ambayo wanatamani kuona yanatimia,” alisema Nabi aliyeipa Yanga Ngao ya Jamii kwa kuifumua Simba bao 1-0 la Fiston Mayele.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.