HAJI MANARA APOROMOSHA MVUA YA MANENO' KWA NABI....,AONGELEA MFUMO ANAOUTUMIA
MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amemsifu kocha wa timu hiyo, Nassredine Nabi kwa namna ambavyo timu hiyo inavyocheza soka lake la pasi nyingi.
Yanga katika mchezo wao uliopita dhidi ya Azam walipiga pasi 23 kuanzia kwa kipa mpaka wachezaji wa mbele na Jesus Moloko aliweka wavuni bao la pili.
Manara amesema mpaka sasa katika timu yao wachezaji wao wote wanapiga pasi na hilo lilianza kujitokeza katika mchezo wao dhidi ya KMC
“Tunacheza PPP yaani Piga pasi, Pokea na Pita mbele na hii imeanza kujitokeza katika mchezo wa Kmc lakini hata mchezo wa juzi bado tumeendelea,” amesema Manara.
Msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi amesema anamsifu kocha Nabi kwa kuitengeneza timu hiyo na sasa kucheza soka safi na la kuvutia.
“Nabi ni Profesa ameifanya Yanga kupiga pasi nyingi wakati huo huo timu ikipata ushindi, kumpongeza ni lazima kwa kazi anayoifanya.”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: