KIMEUMANA! SIMBA IKIPITIA WAKATI MGUMU BERNARD MORRISON AIBUKA NA JIPYA TENA KAMBINI
MSHAMBULIAJI wa Simba, Bernard Morrison kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kwa wakati huu ambao wanapitia wapinzani wao (Yanga) lazima watakuwa wanafurahia kwa sababu ndivyo mpira ulivyo.
Morisson aliandika ; "Muda mwingine mpira unaweza kutoa maumivu makali na mambo mazuri pia, mechi yetu na Jwaneng Galaxy umetuletea huzuni lakini ni furaha kwa wapinzani wetu, huu ndio uzuri wa mpira wa miguu."
Mshambuliaji huyo pia amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa nao pamoja licha ya kuwa kwenye wakati mgumu mpaka sasa.
"Ni mpito tu, tuungane na mambo yatakuwa sawa, tumekuwa hivi kwasababu yenu hivyo msituache".
Simba imejikuta ikiwa na wakati mgumu baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia hata kwenye Ligi wamekuwa na muenendo mbaya baada ya kuchezesha mechi nne wakishinda miwili na sare mbili.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: