INSHU YA KOCHA MPYA SIMBA YAFIKIA HAPA, HII NDIO TAREHE ATATANGAZWA RASMI

Ukweli ni kwamba Simba juzi asubuhi wamezungumza na kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena kama miongoni mwa watu wanaoweza kurithi mikoba iliyoachwa na Didier Gomes Da Rosa.

Hata hivyo urefu wa mkataba wa kocha huyo na uwekezaji wa Mamelodi Sundowns pamoja na kiasi kikubwa cha fedha anacholipwa ni mambo ambayo bila shaka yataipa Simba ugumu wa kumnyakua ingawa habari za ndani zinasema anapenda sana kuja Msimbazi atengeneze wasifu mpya.

Kwa mujibu wa takwimu za gharama zake kwenye miaka ya hivikaribuni, ikiwa Simba ina nia hasa ya kumnyakua Mokwena, inapaswa kutenga kiasi kisichopungua Sh 1.2 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya kumlipa mshahara tu kocha huyo, fedha ambayo haijumuishi posho, bonasi na stahiki nyingine ambazo zikijumuishwa anaweza kuigharimu zaidi ya Sh 1.3 bilioni kwa mwaka.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari huko Afrika Kusini, mshahara wa mwezi kwa Mokwena hivi sasa ni kiasi cha Randi 650,000 ambacho ni takribani Sh 98 milioni kwa thamani ya fedha ya Tanzania.

Hii inamaanisha kuwa kwa miezi 12, Simba itapaswa kumlipa Mokwena kiasi cha Sh 1.17 bilioni kwa ajili ya mshahara tu. Ingawa watu wa Simba wamesema kwamba hiyo ishu ya stahiki zake ina utofauti kidogo na iliyoko mitandaoni.

Lakini kana kwamba haitoshi, Simba italazimika kulipa kiasi kikubwa cha fedha takribani Dola 260,000 (zaidi ya Sh 600 milioni) ili kuvunja mkataba wa Mokwena mwenye umri wa miaka 34.

Jambo la tatu ambalo kifedha linaongeza ugumu kwa Mokwena kujiunga na Simba ni ubora wa kikosi cha Mamelodi Sundowns na mazingira mazuri zaidi ya ufundishaji aliyonayo hapo ambayo yanamuweka katika nafasi nzuri ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika tofauti na Simba ambayo haijawa na uwekezaji mkubwa.

Kudhihirisha hilo, hivi karibuni kocha huyo alinukuliwa akielezea kukoshwa na sapoti na mazingira mazuri ambayo yeye na benchi lake la ufundi wamekuwa wakipata ndani ya Mamelodi akitaja kama ndio chachu kubwa ya wao kufanya vizuri “Pongezi za kipekee kwa Rais, mwenyekiti, familia ya Motsepe na bodi ya klabu kwa sapoti kubwa ambayo mmekuwa mkitupa. Haya yasingewezekana bila imani kubwa ambayo mmeiweka kwetu,” alisema Mokwena.

WAMEBAKI WATATU

Jopo maalumu linalosimamia mchakato wa kutafuta kocha mpya siku nzima ya jana lilikuwa na kikao cha kuhitimisha kuwapata makocha wapya watatu ambao siku si nyingi watatua nchini.

Mokwena ni miongoni mwa waliopita katika mchujo lakini amefanyiwa mahojiano na jopo hilo jana asubuhi.

Mokwena katika mahojiano hayo amepita katika sifa na vigezo vyote ambavyo Simba walikuwa wanahitaji katika kumpata kocha mpya vikiwemo, kuchukua ubingwa wa Ligi ya mabingwa Afrika na leseni A ya CAF,

Baada ya mahojiano hayo yaliyofanyika kwa njia ya zoom, kumalizika jopo hilo liliendelea na mchujo wa makocha wengine ili kuwapata ambao wataingia tatu bora na mmoja kati ya hapo ndio atapewa kazi.

“Tutampata kocha mkuu mara baada ya mechi na Namungo kisha ataanza kazi wakati ligi imesimama kutokana na ratiba ya timu ya taifa hapo atakuwa na muda wa maandalizi ingawa wachezaji wote hawatakuwepo,”alidokeza kigogo mmoja wa Simba.

“Kuna kocha mmoja wa Afrika ameomba kazi na tumeanza kufanyia kazi wasifu wake kama utakuwa vile ambavyo tunahitaji tutafanya nae kazi lakini kuna wengine hawakuomba nao tunawafuatilia,” alisema Barbara.

“Tunahitaji kocha ambaye hatakuwa na wasifu mkubwa mno kwani atakuwa na malengo ya kupata mafanikio na kuongeza ubora wake kwa kuchukua mataji na kufanya vizuri kupitia Simba.”

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.