HABARI MBAYA KWA SIMBA, WACHEZAJI HAWA MUHIMU KUIKOSA MECHI DHIDI YA NAMUNGO
Kiungo wa klabu ya soka ya Simba, Mzamiru Yassin atakosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Namungo baada ya kupata majeraha kwenye mtanange uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Yassin anaongeza idadi ya majeruhi kwenye kikosi cha wekundu wa Msimbazi ambapo Kocha Msaidizi Selemani Matola, ameweka wazi kuwa Chris Mugalu, Taddeo Lwanga pamoja na Pape Ousmane Sakho nao wataendelea kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha yanayowakabili.
Katika hatua nyingine, Matola amesema kuwa wanakosa muda wa kujiandaa kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku mbili hivyo kupelekea ugumu kwenye kurekebisha makosa yao yaliyojitokeza kwenye mechi iliyopita huku akitabanaisha kuwa hawana budi kucheza michezo hiyo kulingana na ratiba ya Ligi kuu ilivyopangwa.
Pia mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars amekiri kuwa wanapitia katika kipindi kigumu kinachogubikwa na kukosa matokeo na kusema kuwa wanaimani kubwa ya kutetea ubingwa wao msimu huu, kutoka na kuwepo na kundi la wachezaji wengi waliopitia nyakati kama hizi msimu uliuopita.
Vilevile kwa upande wa Jangwani, Yanga itamkosa kiungo mchezeshaji Khalid Aucho kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting katika dimba la Mkapa kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: