JAMAA ANASWA LIVE AKIFANYA MAPENZI NA MBUZI...AELEZA POLISI KUWA 'ALIZIDIWA TU NA HAMU'

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera kamishna msaidizi wa polisi Jumaa Awadhi, kulia ni picha mnyama mbuzi (siyo wa kwenye habari)

Na Ashura Jumapili,Kagera.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linamshikilia Emmanuel Zakaria (38) Mkazi wa Lusahunga Wilayani Biharamulo Mkoani humo kwa kosa la kufanya mapenzi na mbuzi jike mali ya Jacobo Nyawenda (37).

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera kamishna msaidizi wa polisi Jumaa Awadhi amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24,2021 majira ya saa tisa alasiri katika kijiji cha Lusahunga kata na tarafa ya Lusajunga wilayani Biharamulo ambapo mtuhumiwa Emmanuel Zakaria ,alimchukua Mbuzi huyo aliyekuwa amefungwa malishoni kisha kumpeleka vichakani na kuanza kufanya naye mapenzi .

Amesema wakati akiendelea na kitendo hicho ,ndipo alipita mke wa jirani yake na mlalamikaji na kumkuta mtuhumiwa anafanya mapenzi na mbuzi akatoa taarifa kwa wananchi wengine na mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi na wananchi hao.

Kamanda Awadhi amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi alikiri kufanya tukio hilo na kudai kuwa alizidiwa na tamaa za mwili. .
Amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na kwamba mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kituo cha polisi Biharamulo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.