CAF YATOA ROPOTI HATMA YA BIASHARA UNITED
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika kupitia tovuti yake ya Cafonline.com imethibitisha kuwa bado uamuzi wa mechi ya marudiano kati ya Ahly Tripoli na Biashara United haujatolewa.
Jana saa nane mchana droo ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ilifanyika kule Cairo Misri kunako makao makuu ya CAF, ambapo timu 16 zilizofuzu raundi hiyo ya pili zilipangwa na timu 16 zilizotolewa kwenye ligi ya mabingwa Afrika.
Hata hivyo orodha ya CAF CC ilikuwa ina timu 15 tu ambapo timu 1 ya 16 itatokana na uamuzi wa CAF kuhusiana na hatma ya mechi ya Ahly Tripoli na Biashara United.
Timu zilizofuzu ni RS Berkane(Morocco),JS Kabylie (Algeria), Enyimba (Nigeria) ,SC Sfaxien (Tunisia), JS Saoura (Algeria), Pyramids (Misri), Al Masry (Misri), Gor Mahia (Kenya), Marumo Gallants (Afrika Kusini), Coton Sport (Cameroon), Orlando Pirates (Africa Kusini), Red Arrows (Zambia).
Nyingine ni DC Motema Pembe,(DR Congo), Binga Fc (Mali), CD Inter clube (Angola), Tusker (Kenya), Hearts of Oak (Ghana), Stade Malien (Mali), LPRC Oilers (Liberia),US Gendarmerie Nationale (Niger), Al Itthad (Libya),, APR (Rwanda).
Vilabu vingine vilivyofuzu hatua hiyo ni pamoja na AS Maniema Union(DR Congo),TP Mazembe (DR Congo), Simba(Tanzania), Rivers United(Nigeria), ASEC Mimosas (Ivory Coast), AS Otoho( Congo), FC Nouadhibou(Mauritania), Royal Leopard (Eswatini), Zanaco (Zambia.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: