AZAM FC WAWAOGOPESHA WASOMALI
KABLA ya mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Septemba 18, kati ya Horseed FC ya Somalia dhidi ya Azam FC ya Tanzania. Tayari Wasomali hao wameanza kuingia hofu juu ya Azam FC.
Katika mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao huo ulisoma Azam FC 3-1 Horseed FC hivyo mchezo wa marudio unatarajiwa kuwa wa kukata na mundu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Horseed FC, Mohamed Hussein Ahmed alisema kuwa kwa namna alivyowaona Azam FC kwenye mchezo wa kwanza ni lazima atafute mbinu mpya kuweza kushinda.
“Walitufunga mchezo wa kwanza kutokana na makosa ambayo tuliyafanya, ipo wazi walituzidi katika mbinu kwa kuwa ni timu bora lakini haina maana kwamba mchezo ujao tutawahofia.
“Tumejua kwamba ni wazuri kwa mipira iliyokufa hata mabao ambayo wametufunga asilimia kubwa yametokana na mpango huo hivyo tutaufanyia kazi ili kupata matokeo,” alisema Ahmed.
Azam FC itamenyana na Horseed FC, Septemba 18 Uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa marudio.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: