YANGA WAPEWA TAHADHARI HII KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA WANAIGERIA, WAKIFANYA HAYA WATATOBOA


Timu ya wananchi yanga African sports club, inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ambao walianza kufanya kazi mbele ya Rivers United ya Nigeria na mchezo huo uliochezwa bila ya mashabiki kama ilivyokuwa kwa Azam FC.

Ulikuwa ni mchezo mzuri kwa Yanga na mbaya kwa mashabiki kwa kuwa hakuna ambaye alitarajia kile kitatokea.

Kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ni maumivu kwa mashabiki huku Yanga wao wakiwa kwenye nafasi nzuri ya kuona makosa yao na wanatakiwa kuyafanyia kazi ili waweze kushinda.

Wachezaji pamoja na benchi la ufundi hakuna haja ya kukata tamaa kwa muda huu kwa kuwa nafasi ipo ikiwa makosa yatafayiwa kazi.

Huu ni mpira na kila timu inastahili kushinda hivyo hakuna timu ambayo inapaswa kufungwa wala ambayo inapaswa kushinda muda wote.

Ikiwa hivyo basi isingekuwa na umuhimu wa kuwepo kwa mechi basi zile timu ambazo unadhani zinastahili kushinda zingekuwa zinakaa pembeni na kuziacha timu nyingine kushiriki. Kwa kuwa ni mpira basi ni lazima mchezo uchezwe.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.