YANGA BADO WANA NAFASI NZURI
Pamoja na Yanga kutoka sare ya mabao 2-2 na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Ijumaa, bado wanajangwani hao wana nafasi ya kumaliza nafasi ya pili, Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambao sare yao imewafanya kufikisha pointi 52 na kukaa kwenye nafasi ya tatu, wanahitaji ushindi wa aina yoyote mbele ya Azam wenye pointi 55. Ushindi huo utaishusha Azam ambayo ipo nafasi ya pili.
Mchezo wa mwisho ambao utaikutanisha miamba hiyo miwili kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, utaamua hatma ya nani atamaliza kwenye nafasi hiyo baada ya Simba kutangaza ubingwa.
Kama Yanga itaifunga Azam kwa ushindi wowote watakuwa wamefikisha pointi 55 sawa na Azam, kitakachowabeba ni kanuni ya utofauti wa mabao ya kushinda na kufungwa.
Hata kanuni ya matokeo ya baina yao kwenye michezo ya duru la kwanza na la pili ‘Head to Head’ itaifanya Yanga kumaliza kwenye nafasi ya pili.
Yanga iliifunga Azam kwenye mchezo wa duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mabao 2-1,Januari 27 mwaka huu.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: