SIMBA SC YABADILISHA RATIBA YAKE YA MAZOEZI
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2017/18 Simba SC, imebadili ratiba yake ya kuanza mazoezi baada ya kuwapa mapumziko wachezaji wake kufuatia kusimama kwa ligi.
Kikosi cha Simba SC sasa kitaanza mazoezi yake rasmi siku ya Jumatatu kwenye viwanja vya Polisi Jijini Dar es Salaam. Awali taarifa ya klabu ilieleza kuwa timu ingeanza mazoezi ijumaa hii.
Simba itakuwa inajiandaa na mchezo wake wa raundi ya 12 ligi kuu soka Tanzania Bara, ambapo itakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) imesimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la CECAFA Challenge inayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: