MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI JOSHUA NASSARI AVAMIWA USIKU WA KUAMKIA LEO
Watu wenye silaha wamevamia nyumbani kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe.Joshua Nassari maeneo ya USA River, usiku wa kuamkia leo na kufyatua risasi kadhaa ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nyumbani hapo.
Nassari na mkewe walifanikiwa kutoroka, kisha kuripoti tukio hilo Polisi. Kamanda wa Polisi Arumeru, amesema wanafanya uchunguzi kubaini watu hao.
Haya ndiyo maneno ya Joshua Nassari kupitia ukurasa wake wa Twitter
Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi.
Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: