MAKALA: SONONEKO LA NINI YANGA?

ANAANDIKA PASCAL KABOMBE
Siku ya tarehe 3 itabaki kukumbukwa na wana simba pamoja na wanamichezo kama siku ya mapinduzi ya kimfumo, kiuongozi na kiuendeshaji wa timu kwenye soka la Tanzania, hakika ni jambo jema na la kuigwa mfano na jamii yoote ya wapenda soka Tanzania kwa mustakabali wa soka la nchi yetu.

NANI HASA ALILIONA HILI JAMBO JEMA?

Jibu ni rahisi sana,
YANGA......... NDIO NI YANGA. Katika ukanda wetu huu wa CECAFA ni timu ya Yanga iliyokuwa na viongozi wenye weledi mkubwa na kuona inafaa klab kuwa na Kampuni kwa ajili ya uwekezaji na kutoka katika mfumo wa sasa wa timu kumilikiwa na wanachama....

USHAHIDI UPO??
Miaka ya 90 kiongozi wa Yanga Bwana George Mpondela (Castro) aliliona hili na akalipendekeza kwa wanachama wa Yanga.... Kilichotokea nchi nzima inajua, wanachama waligoma wakidhani wanaporwa timu, yaani hili jambo wanalofanya simba wenzao Yanga kwakutokujua walilikataa miaka 20 iliyopita.

Mfano mwingine ni wa aliyekuwa kiongozi wa Yanga (sasa ni mwenyekiti wa bodi ya kubahatisha)Bwana Abbas Tarimba na yeye aliliona hili na akalipendekeza... Kilichotokea Africa nzima inajua, wanachama waliona wanaporwa timu.

Na katika nyakati tofauti waliounga mkono waliitwa Yanga kampuni na waliopinga waliitwa Yanga Asili. Na katika minyukano hiyo Yanga asili ilishinda ikiibuka kidedea na kushangiliwa na wanachama wengi sana.

Sasa Simba wameanza na kufanikiwa kupiga hatua, Yanga wanasononeka nini? Hili jambo lilikuwa lifanikiwe tangu Rais wa nchi ni Mkapa lakini watu wakakataa.

Manji alipotaka "Kukodi" badala ya kuweka masharti watu wakakataa.

Leo sononeko linatoka wapi? Kupanga si kuchagua? Majaribio matatu yote yamegonga mwamba kwa miaka 20, yaani Mpondela, Tarimba na Manji, jaribio moja la Simba ..... mpira umeenda nyavuni.

Leo hii Simba inajitapa (ni haki yao) kuwa ya kwanza kubadili mfumo.. Lakini Yanga imetimiza miaka 20 sasa ikikataa mfumo.

SASA WAKUBALI WALICHOKATAA KWA MIAKA 20 AU WASUBIRI MIAKA MINGINE 20?

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.