MAJEMBE YA SIMBA YARUDI RASMI


KIKOSI cha Simba jioni ya leo kitashuka Uwanja wa Azam Complex kuvaana na KMC, lakini kama kuna kitu kinachowafurahisha benchi la ufundi ni kitendo cha kurejea uwanjani kwa majembe yao yaliyokuwa majeruhi.

Kipa Mohammed Said ‘Nduda’ na beki wa kati, Salim Mbonde wanatarajia kurejea tena uwanjani kuungana na wachezaji wenzao Jumatatu wakati kikosi chao kitakapokuwa kikianza tizi la ufukweni kabla ya kuhamia gym.

Nyota hao walikuwa wakisumbuliwa na magoti, lakini Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema ameshawasiliana na daktari aliyekuwa akiwatibu wachezaji hao na kutoa ruksa waanze kujifua taratibu si chini ya dakika 40.

Gembe alisema wachezaji wote wataanza tizi la ufukweni na watawajumuisha Mbonde na Nduda japo watafanya ya peke yao.

“Majeruhi pekee aliyesalia kikosini ni Shomary Kapombe, lakini Mbonde na Nduda wataanza mazoezi Jumatatu,” alisema Gembe.

Naye Kocha Msaidizi, Masudi Djuma alisema wanataka kuanza mazoezi ya ufukweni kuongeza stamina kabla ya kuwafuata Ndanda.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.