KOCHA WA SIMBA AAMUA KUVUNJA LIKIZO NA KUMFUATA MAGURI KENYA

Kocha wa Simba, Joseph Omog sasa yupo mapumziko kwao Cameroon lakini ameamua kusitisha mapumziko yake ghafla na kutaka kwenda Kenya kumtazama straika Elias Maguri ili aweze kumsajili.

Simba inataka kuboresha kikosi chake kwa kusajili beki mmoja na straika mmoja atakayeingia moja kwa moja kikosi cha kwanza, Maguri anayechezea Dhofar SC ya Oman anatajwa kuwa katika rada za klabu hiyo.

Kwa sasa Maguli aliyewahi kuchezea Ruvu Shooting, Stand United na Simba, yupo Kenya katika kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kinachoshiriki Kombe la Chalenji.

Michuano ya Kombe la Chalenji inaanza kesho Jumapili ambapo Kilimanjaro Stars itaanza kucheza na Libya huku ikifuatiwa na mchezo mwingine kati ya wenyeji, Kenya na Rwanda.

Kutoka Cameroon, Omog amesema ameuomba uongozi umpeleke Kenya kutazama viwango vya wachezaji kabla
ya kutoa mapendekezo ya kumsajili mchezaji yeyote katika usajili huu wa dirisha dogo.

Omog alisema, kikosi chake kinahitaji baadhi ya marekebisho na hataki kubahatisha katika usajili wao, hivyo wanahitaji mshambuliaji mmoja atakayeingia kikosi cha kwanza moja kwa moja.

“Hii ni nafasi pekee kwangu kama kocha kwenda kuangalia wachezaji katika michuano hii ya Chalenji kuliko kumuita mchezaji katika timu kwa ajili ya kumfanyisha majaribio.

“Kama mambo yakienda vizuri basi nitaenda Kenya kwa ajili ya kuangalia michuano hiyo ambayo kwangu ninaiona ina umuhimu mkubwa,” alisema Omog.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Simba alikiri kupokea ombi hilo la Omog na kusema wanalifanyia kazi haraka ili kocha huyo aweze kwenda Kenya kutazama mechi za Chalenji.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.