Tanzia: MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI ESTHER ISAAC NGALALA AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MOCU) Kituo Cha kufundishia Kizumbi Esther Isaac Ngalala afariki dunia leo alfajiri baada ya kuugua kwa muda mfupi
Taarifa zilizotufikia kutoka kwa mtu wa karibu na familia ya Esther, Esther alianza kuugua akiwa chuoni Kizumbi Shinyanga tangu Jumatano akisumbuliwa na uvimbe shingoni na ambapo alilazwa katika zahanati ya Kambarage mjini Shinyanga kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga ambapo iligundulika kuwa ana tatizo la ini hivyo ilibidi kupelekwa katika hosptali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza ambako ndani ya masaa 12 alifariki dunia
Akizungumza na Masengwa Blog jioni hii makamu wa rais wa Chuo Cha Ushirika Moshi Benedict Deograthius Nyoni, amesema kuwa mwili wa marehemu Esther utaagwa kesho tarehe 16/11/2017 hapo chuoni Kizumbi Shinyanga, na baadae utaagwa Lubaga Shinyanga alikokuwa anaishi kabla haujasafirishwa kwenda Mwanza kwa ajili ya mazishi.
"Mwili wa marehemu Esther utawasili hapa chuoni kesho ingawaje muda haujajulikana, ili wanafunzi wote washiriki kumuaga mwanafunzi mwenzao. Nawsihi wanafunzi wote kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwanafunzi mwenzetu, najua ni vigumu kukabiliana na hali hii lakini wajipe moyo kwani haya tumeumbiwa wote" alisema makAmu wa rais wa chuo hicho.
Esther alikuwa akisoma DIPLOMA IN MICROFINANCE MANAGEMENT (DMFM1) mwaka wa kwanza katika Chuo Cha Ushirika (MOCU) Kituo cha kufundishia Kizumbi Shinyanga
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: