JE, UNAMFAHAMU MCHEZAJI WA YANGA ANAYEOGOPWA KWENYE MECHI YA LEO NA SINGIDA UNITED? HUYU HAPA SASA

MKURUGENZI wa Klabu ya Singida United Festo SANGA amemtaja mchezaji ambaye wao kama Singida United wanamhofia kuelekea Pambano la Leo kati ya Singida United na Yanga mchezo unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Namfua Kuanzia Majira ya Saa Kumi Jioni.

Sanga amesema wao kama Singida United wanamhofia zaidi Papy Kabamba Tshishimbi katika mchezo wa Leo.

“Sisi kama uongozi tumejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo lakini pia mambo yote ya kiufundi ndani ya uwanja, pia ko­cha wetu, Pluijm amejipanga vizuri.

“Hata hivyo, mchezaji ambaye tunam­hofia zaidi kwa upande wa Yanga ni Tsh­ishimbi kwani ni mchezaji mzuri tangu amejiunga na timu hiyo ndiye injini yao, tukifanikiwa kumdhibiti huyo basi kazi itakuwa nyepesi kwa upande wetu,”Alisema Sanga Mkurugenzi wa Singida United
Mechi ya Mwisho iliyozikutanisha Yanga na Singida United ilikuwa ni ile ya Kutest Mitambo Mwaka Huu kalbla ya Ligi Yanga ikiibuka na Ushindi wa Bao 3 kwa 2 mechi ikichezwa uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.