LULU ATIMUA MBIO MAHAKAMANI...BABA YAKE AWA BODIGADI WAKE
Tukio hilo la Lulu kuwakimbia waandishi wa habari limetokea baada ya Shahidi wa pili upande wa utetezi ambaye ni mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbushi, ambaye ameshindwa kufika mahakamani hapo leo hii kwa ajili ya kutoa ushahidi wake kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa yupo nje ya nchi na hakuweza kupatikana moja kwa moja.
Baba Lulu amekimbizana na waandishi wa habari mpaka kwenye gari analolitumia mwanae na kukaa mbele ya gari kuwaambia waandishi waliokuwepo hivi “Leo picha hampigi tafadhali mwiza maekata kata watu na viroba hampigi picha mmechimbi chini huyu mnamfuata leo hampigi picha,” hayo ndio baadhi ya maneno yaliyosikika kwa baba Lulu.
Hata hivyo mashabiki wa msanii huyo walianza kuwalaumu waandishi wa habari, kwa kusema kuwa ” Kwanini mmetuondolea Lulu wetu ilibaki kidogo aanguke na angeanguka mngempiga picha mngetukoma,” hayo ni maneno ya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo kwa waandishi wa habari.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi