HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO IJUMAA OCTOBER 27, 2017
Ligi Kuu Tanzania VPL leo Ijumaa 27.10.2017 itaendelea kwa mhezo mmoja kati ya Azam Fc watakaoikaribisha Mbeya City Pale Azam Complex Chamazi ambao ndiyo uwanja wa Nyumbani wa Azam Fc.
Mchezo huo wa raundi ya 8 ya Ligi Kuu VPL 2017/2018 utaanza majira ya saa moja jioni ya leo, Azam Fc inaingia katika mchezo wa Leo ikitafuta ushindi mara baada ya kubanwa na Sare katika mechi zake 3 zilizopita wakati Mbeya city ikiingia katika mchezo wa leo ikijivunia ushindi ilioupata mchezo uliopita ikiiminya Ruvu Shooting bao 2 kwa 0 Sokoine Stadium.
Azam wapo nafasi ya 4 katika msimamo ikiwa na Points 13 wakati Mbeya City wakiwa nafasi ya 6 wakiwa na points 12 mara baada ya timu zote kucheza michezo 7.
Chanzo-kwataunit.com
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi