HABARI MPYA NA ZA KUSISIMUA KUTOKA YANGA ASUBUHI YA LEO IJUMAA OCTOBER 27, 2017

Klabu ya Yanga leo Oktoba 27 wametangaza kuanza rasmi kuuza jarida la Klabu yao maarufu kama "Yanga Magazine" Yanga ambayo ndiyo klabu kongwe zaidi Tanzania ikianzishwa mwaka 1935 imeamua kutoa jarida hilo litakalokuwa linaandika mambo mengi kuhusu Klabu hiyo inayotokea mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kupitia Ukurasa wa Yanga wa Twitter wameandika kuwa Jarida hilo litaanza kuuzwa kuanzia majira ya asubuhi ya leo saa 3 asubuhi.

Yanga Magazine itaanza kuuzwa rasmi kesho kuanzia saa 3:00 Asubuhi Makao Makuu ya Klabu
Zaidi wasiliana na Idara ya Habari - 0757569752
Yanga Magazine itaanza kuuzwa rasmi kesho kuanzia saa 3:00 Asubuhi Makao Makuu ya Klabu
Zaidi wasiliana na Idara ya Habari - 0757569752


SHUJAA AMERUDI,SHUJAA YUKO NYUMBANI
Moja kati ya sehemu ambazo zinaweza kuwa kivutio Kikubwa Katika jarida hilo ni ile sehemu ambayo imeandikwa SHUJAA AMERUDI,SHUJAA YUKO NYUMBANI Huku kukiwa na picha za mwenyekiti wa zamani wa Klabu hiyo Mfanyabiashara Yusuph Manji.

Imekuwa ikisemekana tu kuwa Manji amerejea lakini haijawahi kuwekwa wazi na Uongozi sasa huenda kwenye jarida hili linaloanza kuuzwa leo Ukweli ukawekwa wazi kupitia kiapnde hiko.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.