HAJI MANARA HAISHIWI VITUKO...AMCHIMBA MKWARA MZITO IBRAHIM AJIBU




Kuelekea mechi dhidi ya Yanga itakayochezwa leo Jumamosi 28.10.2017, Ofisa habari wa Simba, Haji Manara ametoa kauli nyingine inayoonekana ni kitisho kwa wapinzani wao, Yanga.Manara ambaye anajulikana kwa kuwa na maneno mengi ya utani wa kisoka, ameonyesha wazi kumlenga Ibrahim Ajibu wa Yanga licha ya kuwa hajamtaja jina.

Katika ujumbe wake wa Instagram, Manara ameandika hivi: “Anaitwa Juuko Murshid, ni beki asiyecheka uwanjani, na ni jitu katili hasa, sasa mchuzeeni tu, anamjua vizuri sana, Salah wa Misri anajua kazi yake, kwa sasa Juuko ndiyo defender bora wa kati EA.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.