HABARI MPYA ZILIZOJIRI HIVI PUNDE KUHUSU MECHI YA YANGA NA SIMBA KESHO

SIMBA
Klabu ya Simba ambayo ipo Visiwani Zanzibar ikifanya maandalizi ya Mwisho visiwani humo inatarajiwa kuingia Dar Es Salaam siku ya kesho huku ikitumia usafiri wa Ndege kutokea Zanzibar na kuingia mjini Dar na Itafikia hotelini siku hiyo hiyo ya Kesho kabla ya kuelekea uwanjani kupambana na Yanga.

Simba ambayo jana ilionekana ikifanya mazoezi kwenye mvua inaelezwa kambi yao iko shwari na mipango yote iko sawa.

YANGA
KLABU ya Yanga ambayo iliweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mechi dhidi ya Mtani wake wa Jadi Simba, leo mchana timu hiyo itaondoka mjini Morogoro na kurejea jijini Dar Es Salaam kwaajili ya mchezo wa Kesho uwanja wa Uhuru.

Yanga inaondoka Morogoro baada ya mazoezi ya asubuhi ya leo huko Morogoro ilipokuwa imeweka Kambi ya siku kadhaa toka siku ya Jumanne.

Yanga msomaji wa Kwataunit.com itaondoka mchana wa leo kwa usafiri wa basi lao huku taarifa zikieleza kuwa watafikia kwenye hoteli katikati ya jiji (Hoteli haijatajwa), Yanga wataondokea hoteli hiyo hapo kesho kuelekea uwanjani kumenyana na Simba.

Yanga na Simba kesho zitaisimamisha Nchi hususani kwa wapenzi wa Soka kuanzia majira ya saa kumi jioni ambao ndiyo muda wa mechi hiyo Kuanza.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.