WAZAZI WANAOFUNGIA WATOTO NJITI MAJUMBANI WAONYWA



WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amewataka wanawake wanaojifungua watoto njiti kuwathamini watoto wao, kuwatunza na kuwapatia fursa ya elimu ili waweze kufikia ndoto za maisha yao badala ya kuwafungia majumbani.
Waziri Kairuki aliyasema hayo jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Jumuiya ya Wanawake(UWT) wa Chama Cha Mapinduzi, wakati akitoa msaada wa vitanda na zawadi mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni nane kwa wanawake wa wodi ya Kangaroo katika hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

“Nimekuja kuwasalimu, kuwatia moyo na kusherehekea pamoja siku ya wanawake duniani… Mimi mwenyewe ni njiti, nilizaliwa njiti na ninafahamu kila kitu kwa kuwa nami nilipitia mazingira ya njiti, hivyo niwatoe hofu kwa kuwa bado nipo na nina akili za kutosha, natumikia taifa langu na natekeleza majukumu yangu bila shida, kwa vyovyote na watoto mlionao sasa wataweza kufika mbali,” alisema.


IMEANDIKWA NA HELLEN MLACKY WA HHABARI LEO 

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.