SHEHENA YA POMBE YA VIROBA YAZUIWA NA SERIKALI DAR ES SALAAM
Marufuku ya pombe aina ya viroba ilitolewa na waziri mkuu mapema Feb 16 akiwa Mererani mkoani Manyara ambapo maafisa wa serikali wanasema wanalitekeza agizo hilo kikamilifu na kwa mujibu wa sheria.
Oparesheni hiyo ya kuondoa pombe aina ya viroba imehusisha maafisa kutoka taasisi mbalimbali za serikali ambapo wanasema faini ya 50000 hadi kifungo cha miaka 3 jela huenda vikawakabili watakaokiuka agizo la waziri mkuu ambalo limeanza kutelezwa mapema March Mosi mwaka huu.
Lakini kwa mujibu wa meneja wa kanda wa kampuni ya Mega trade ambao ndio wamiliki wa shehena hiyo anasema shehena hiyo ilifungiwa na maafisa wa TFDA tangu mwaka octoba 2016 huku akiiomba serikali kuona namna wanavyoweza kuwasaidia kuepuka hasara kubwa ambayo wamekwisha kuipata.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi