Waliomua mtu na kumweka kwenye 'kiroba' wafikishwa mahakamani


Moshi. Wakazi wawili wa mjini Moshi,wamefikishwa kortini kwa tuhuma za kumuua mtu mmoja, kisha kuweka mwili wake kwenye mfuko wa Sandarusi na kuuchoma moto kwa kutumia petroli.

Watuhumiwa hao ni mfanyakazi wa ndani wa watuhumiwa wawili wanaosakwa na Jeshi la Polisi, Jonasia Aloyce au Masilayo (48) mkazi wa Majengo.

Mwingine aliyefikishwa mahakamani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Juliet Mawole, ni Humphrey Manongi (36) anayetuhumiwa kushiriki kubeba mwili wa marehemu na kuungiza kwenye gari.

Akiwasomea mashtaka hayo, wakili wa Serikali,Kassim Nasri alidai Desemba 13, mwaka jana katika eneo la Majengo Savena katika Manispaa ya Moshi, washtakiwa walimuua kwa makusudi Steven Kimario(55).

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji isipokuwa Mahakama Kuu na kesi hiyo imepangwa kutajwa Januari 30.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.