ASKOFU DR. EMMANUEL MAKALA AWAOMBA WAZAZI NA WANAFUNZI KUWA MABALOZI WA SHULE YA SEKONDARI MWADUI
Askofu wa KKKT- DAYOSISI KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA (DKMZV), Dr. Emmanuel Makala amewasihi wazazi na wanafunzi kuwa mabalozi wa shule ya Sekondari ya Mwadui kwa kuitangaza shule hiyo ndani na nje ya nchi kwani ni shule ambayo ipo kwa ajili ya kuwafanya vijana kufikia ndoto zao kama wataenda shuleni kwa lengo la kusoma.
Akizungumza katika mahafali ya kuhitimu kidato cha nne iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 01 Oktoba, 2016 shuleni hapo, Askofu Makala (mgeni rasmi) amepongeza juhudi za mkuu wa shule hiyo mchungaji Yohana Nzelu, walimu pamoja na bodi ya shule kwa kuifanya shule hiyo kuwa miongoni mwa shule zilizoingia kumi bora kimkoa mwaka 2015.
Jumla ya wanafunzi 125 wa shule hiyo, wanatarajia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne unaotarajiwa kuanza tarehe 01 Novemba 2016.
Katika hatua nyingine mkuu wa shule hiyo mchungaji Yohana Nzelu, alitoa wito kwa wazazi kuwa shule hiyo imeanzisha kidato cha tano na sita kwa michepuo ya PCB, PCM, CBG, HKL, HGK na tayari wanafunzi wa kidato cha tano wapo shuleni wakiendelea na masomo.
Mahafali hiyo pia ilihudhuriwa na Msaidizi wa Askofu Trafaina Assery Nkya, katibu mkuu wa dayosisi mchungaji Daniel Mono, mkurugenzi wa elimu ya kikristo dayosisi Bi. Grace Mutabuzi, mkurugenzi wa wanawake na watoto Martha Ernest pamoja na maafisa wengine wa dayosisi kusini mashariki ya ziwa victoria.
Shule ya sekondari Mwadui ni shule inayomilikiwa na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania iliyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Mgeni rasmi Askofu Dr. Emmanuel Makala akitoa hotuba fupi
Mgeni rasmi Askofu Dr. Emmanuel Makala akitoa vyeti kwa wahitimu
Msaidizi wa askofu na Dean wa kanisa kuu Trafaina A. Nkya (kushoto) akiwa na katibu mkuu wa dayosisi Mchungaji Daniel Mono
Mgeni rasmi akiwa na mkuu wa shule ya sekondari Mwadui Mchungaji Yohana Nzelu
Wahitimu wa kidato cha nne wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwa makini
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi