KIBU DENIS AJIKOMBOA


MARA ya mwisho Kibu Dennis kufunga ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa Novemba 5 2023 Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga.

Hatimaye Machi 14 2025 Kibu kapachika mabao mawili akitoa pasi mbili za mabao kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ambao unafuta ile gundu ya nyota huyo chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu kukwama kufunga.

Dodoma Jiji inabaki na pointi 27 kwenye msimamo huku Simba ikiwa imefikisha pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 22 msimu wa 2024/25.

Kibu amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90 kugota mwisho akiwa kahusika kwenye mabao manne kati ya sita yaliyofungwa na Simba huku Ahoua akifikisha mabao 12 ndani ya ligi ni kinara wa utupiaji.

Katika mchezo wa leo ni Ellie Mpanzu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 15, Jean Ahoua akatupia mabao mawili dakika ya 21 na 45 huku Steven Mukwala akifunga bao moja dakika ya 47 akiwa ndani ya 18.

Kiungo Kibu Dennis amefunga mabao mawili kwenye mchezo na bao lake la kwanza ni dakika ya 54 kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 na bao la pili katupia dakika ya 69.

Post a Comment

Previous Post Next Post