AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI (M&E) KWA WATUMISHI WA UMMA YAFUNGULIWA JIJINI DODOMA

     

Na mwandishi wetu Dodoma

Awamu ya Pili ya Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Watumishi wa Umma, yamefunguliwa leo tarehe 21 julai, 2025 na Bi. Sakina Mwinyimkuu — Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini ili kujenga utamaduni wa uwajibikaji na utendaji unaotegemea matokeo katika Serikali yetu.

Mafunzo haya, yanayofanyika jijini Dodoma, yamewakutanisha washiriki kutoka wizara, idara na taasisi mbalimbali za Serikali, kwa lengo la kuongeza uwezo wao katika usimamizi wa matokeo, matumizi ya taarifa na takwimu, pamoja na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango.

Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Bi. Sakina amewashukuru CLEAR Anglophone Africa (CLEAR-AA) kutoka Afrika Kusini kwa kuendelea kuwa mdau muhimu na kutoa mafunzo kwa kujitolea kwao ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono safari ya Tanzania ya kujenga mifumo thabiti ya M&E yenye tija na endelevu.

Amesema, Juhudi hizo zinaendana kikamilifu na vipaumbele vya taifa ikiwemo Dira 2050 katika kuimarisha upangaji unaotegemea ushahidi, utekelezaji wa sera, na uwajibikaji wa serikali.

“Kadri tunavyoendelea kuwajengea uwezo watumishi wa umma kwa zana za kisasa za M&E, ndivyo tunavyojenga msingi thabiti wa utoaji bora wa huduma, uwazi, na athari chanya kwa wananchi.” amesema Bi Sakina.



Post a Comment

0 Comments