DEREVA ALIYEIBA MAFUTA YA MIL. 77 AKAMATWA


 Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kumkamata Abubakari Mwichangwe (29), Dereva wa Lori la Mafuta lenye namba za usajili T.661BXW Tela namba T.489 BHC ambaye alikuwa anatafutwa kwa tuhuma za kuiba Mafuta aina ya Dizeli Lita elfu 35 yenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 77 kisha kulichoma moto gari hilo kwa lengo kupoteza ushahidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea Machi 16 mwaka huu katika Kijiji Cha Msimba Wilaya kilosa Mkoani Morogoro barabara ya Morogoro -Iringa

Post a Comment

0 Comments