
Nchini Kenya, Mwanamke aliyetambulika kama Mercy Nyasaka amejiua baada ya kuacha ujumbe mzito kwa ndugu wa karibu kupitia Whatsapp akimuaga na kueleza anayoyapitia, Mercy alifiwa na bintiye miaka miwili iliyopita mnamo Machi 1, 2023, kifo ambacho kilimsababishia huzuni kwa kiasi kikubwa kulingana na machapisho yake mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii haswa Facebook.
Licha ya kufiwa na bintiye Mercy mara kadhaa alichapisha machapisho yaliyoashilia kuhisi kukatishwa tamaa na mwenzi wake, na misukosuko mingine ya maisha ikiwemo na matatizo ya kifedha
Katika ujumbe aliotuma siku ya ijumaa kupitia WhatsApp kwa ndugu yake wa karibu, Mercy alimfahamisha kwamba hawezi kuendelea kuyakabili matatizo ya maisha pamoja na kifo cha bintiye, ikiwa ni pamoja na mkopo wa gari, mchumba aliyemkosa, na mkopo wa KSh300,000 aliokopa kwa kutumia hati miliki ya ardhi kama dhamana.
"Samahani kwa kukukatisha tamaa kwa njia hii lakini wakati utapata ujumbe huu nitakuwa nimeondoka kwa muda mrefu," sehemu ya ujumbe aliotuma Mercy.