BARRICK YAWEZESHA WANAFUNZI VYUO VIKUU MBEYA KUTAMBUA FURSA KUPITIA KONGAMANO LA AIESEC 2026

   

Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mbeya University of Science and Technology ( MUST) Prof. Said Wai akifungua kongamano la AIESEC 2026 lililofanyika katika chuo hicho.
Afisa Mwandamizi wa AIESEC Tanzania, Joshua Samwel akiongea na wanafunzi katika kongamano hilo.
Mhandisi Kiugu James wa Barrick North Mara akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo wakijitambulisha
Picha ya viongozi wa AIESEC na wadhamini.

***
Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na serikali kupitia kampuni ya Twiga, imeungana na wadau wengine kudhamini na kushiriki katika kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Mbeya lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC na kufanyika katika katika chuo Kikuu cha Mbeya University of Science and Technology (MUST).

Kupitia kongamano hilo ambalo kufanyika kila mwaka, wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kati huweza kufahamu taasisi mbalimbali na makampuni nchini yanavyoendesha shughuli zake na kujengewa uwezo wa kujiamini na kujiandaa kikamilifu kuchangamkia fursa zinazojitokeza na jinsi ya kutafuta fursa za ajira katika makampuni makubwa,ubunifu sambamba na jinsi ya kujiajiri na kupata mafanikio kupitia katika taaluma zao.

Wafanyakazi wa Barrick waliobobea katika fani mbalimbali walishiriki kutoa mada za kuwajengea uwezo wanafunzi na kuwaeleza shughuli zinazoendeshwa na Barrick-Twiga nchini ikiwemo mkakati wa kampuni wa kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments