BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MIFUKO 60 YA SARUJI KWA UJENZI WA JENGO LA UPELELEZI POLISI SHINYANGA

Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, akiwa na maafisa wa Benki ya CRDB (kulia), wakikabidhi mifuko 60 ya saruji kwa viongozi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga, ambao ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Kaijage John Ndyanabo, na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (OC-CID) Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu wa Polisi Osward Nyorobi (wa kwanza kushoto)kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga.
Sehemu ya mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi Polisi Wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde -  Shinyanga

Benki ya CRDB imeendelea kuonesha dhamira yake ya kushirikiana na jamii kwa kuchangia mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga.

Akikabidhi msaada huo leo Julai 1, 2026, Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, amesema benki hiyo imeamua kutoa mchango huo kwa kutambua mchango mkubwa wa Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao, jambo ambalo ni msingi muhimu wa maendeleo ya jamii na ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Amesema Benki ya CRDB inaamini kuwa mazingira yenye amani na usalama yanachochea maendeleo ya biashara na utoaji bora wa huduma za kifedha, hivyo benki hiyo imeona ni muhimu kushiriki katika ujenzi wa miundombinu itakayowezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

"Tumekuja hapa kwa ajili ya kukabidhi msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya mwendelezo wa ujenzi wa Ofisi ya Upelelezi Polisi Wilaya ya Shinyanga. Polisi ni wadau wetu muhimu, tumekuwa na mahusiano mazuri nao kwa muda mrefu na tunatambua mchango wao mkubwa katika kulinda usalama wa raia na mali zao," amesema Mwenda.

Ameongeza kuwa Benki ya CRDB ipo tayari kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa ubora uliokusudiwa.

"Tulipoombwa kushiriki katika ujenzi huu, tuliona tuanze na mifuko hii 60 ya saruji. Tupo tayari kushirikiana nanyi ili kuhakikisha jengo hili linakamilika. Tunaamini likikamilika litaongeza ufanisi na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi," amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu wa Polisi Osward Nyorobi, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Shinyanga, ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo, akisema ni ishara ya mahusiano mazuri yaliyopo kati ya taasisi hizo mbili.

Amesema mchango huo utasaidia kuharakisha ujenzi wa jengo hilo ambalo linatarajiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa maafisa wa upelelezi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Kwa niaba ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Shinyanga, ninawashukuru Benki ya CRDB kwa mchango huu waliotupatia kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Upelelezi. Msaada huu unatokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Jeshi la Polisi na Benki ya CRDB. Msituchoke, ujenzi huu ni wa mwendelezo na tukiwafuata tena mtupokee," amesema Nyorobi.
Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu wa Polisi Osward Nyorobi, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya mifuko 60 ya saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu wa Polisi Osward Nyorobi, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya mifuko 60 ya saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, akiwa na maafisa wa Benki ya CRDB (kulia), wakikabidhi mifuko 60 ya saruji kwa viongozi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga, ambao ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Kaijage John Ndyanabo, na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (OC-CID) Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu wa Polisi Osward Nyorobi (wa kwanza kushoto)kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda (kulia), akikabidhi mifuko 60 ya saruji kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Kaijage John Ndyanabo, kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (OC-CID) Wilaya ya Shinyanga, Mrakibu wa Polisi Osward Nyorobi.

Post a Comment

0 Comments