
Msanii chipukizi anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo, Mbusule Boy, jina lake halisi Kelvin Juma, ametambulisha rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Maji ya Moto.”
Ametokea Mwanza na kwa sasa anaishi Dar es Salaam ambako anaendelea kukuza kipaji chake cha muziki kwa bidii.
Mbusule Boy yupo chini ya lebo ya Bank Boys Record inayomilikiwa na Don Cash, ambaye pia ni meneja wake.
Kupitia usimamizi huo, tayari ameachia jumla ya nyimbo sita zinazopatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali.
Mbali na “Maji ya Moto,” nyimbo zake nyingine ni pamoja na Uzuri Wako, Katoto, Nasikia Raha, Unaniumiza na Mimi na Wewe.
Wimbo wa “Maji ya Moto” umetolewa Februari 2026, ukiwa umetayarishwa na Mbusuleba huku mtunzi na mtayarishaji wa mashairi akiwa ni Kelvin Juma mwenyewe.
Msanii huyo amesema muziki kwake ni maisha na pia ni biashara, na amewaomba Watanzania kumpokea na kumshika mkono katika kila hatua ya safari yake ya muziki, akiahidi kuendelea kutoa kazi bora zenye ubunifu na mvuto wa kipekee.
0 Comments