Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amefungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu huku akiwataka kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na Maelekezo mbalimbali ya Tume.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa leo Julai 21, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, yakihusisha Waratibu wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi kutoka Halmashauri mbalimbali, kama sehemu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Jaji Mwambegele amesisitiza umuhimu wa watendaji hao kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu, weledi na kusimamia viapo vyao vya kutunza siri na kujitoa au kutokewa wanachama wa chama cha siasa katika kipindi chote cha uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unaofanyika ni wa haki, huru na unaozingatia misingi ya sheria na demokrasia.
Jaji Mwambegele ameongeza kuwa nafasi ya msimamizi wa uchaguzi ni ya msingi katika mchakato mzima wa uchaguzi, kwani ndiye anayehakikisha taratibu zote zinafuatwa, kuanzia ugawaji wa vifaa, uendeshaji wa shughuli za siku ya kupiga kura, hadi usimamizi wa zoezi la kuhesabu na kutangaza matokeo.
Amewataka watendaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutoa taarifa mapema kwa vyama vya siasa kuhusu utaratibu wa kuwaapisha mawakala.
“Wakati wa kuapisha mawakala, toeni taarifa mapema kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya Tume na kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala,” amesema Jaji Mwambegele.
Mwenyekiti huyo wa INEC pia amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanazingatia usawa kwa vyama vyote vya siasa na kuhakikisha mazingira ya uchaguzi ni salama, shirikishi na yenye amani kwa kila mshiriki, ikiwemo wanawake, vijana na makundi maalum.
Washiriki wa mafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Aidha amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka Tume, wanavihakiki, kuvikagua na kuhakikisha vinasambazwa kwenye vituo vyote na kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema.
Amewataka kuhakikisha kuwa siku ya uchaguzi wanaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 kamili asubuhi na kufanya mawasiliano na Tume pale ambapo ushauri utahitajika kuhusiana na masuala ya uchaguzi.
Tume imeyagawa mafunzo hayo kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya pili inahusisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Mwanza, Mara, Dar es Salaam, Pwani, Rukwa, Katavi, Manyara, Arusha, Songwe na Mbeya.
Awamu ya kwanza ilifanyika tarehe 15 hadi 17 na ilihusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.
Mafunzo hayo yanajumuisha mafunzo ya sheria ya uchaguzi, maadili ya uchaguzi, matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi, pamoja na namna bora ya kushughulikia changamoto au malalamiko yatakayojitokeza katika vituo vya kupigia kura.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na mafunzo ya aina hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyika kwa mafanikio makubwa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo kutoka majimbo yote ya Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo pia alitoa mada.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo pia alitoa mada.
Washiriki wa mafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo kutoka majimbo yote ya Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
0 Comments