BAADA YA KICHAPO KWA MKAPA, YANGA YAIFUATA NAMUNGO KWA HASIRA

Baada ya klabu ya yanga kuchezea kichapo kwa mabao 2 kwa bila hapo juzi dhidi ya wababe wao AL HILAL ya Sudan katika mechi ya kwanza hatua ya makundi klabu bingwa Afrika, leo hii wameifuata Namungo FC ya Ruangwa kwa ajili ya mechi ya ligi Kuu NBC Tanzania bara.

Mechi hiyo itachezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 30/11/2024 katika uwanja wa Kasimu Majaliwa kwenye majira ya saa moja usiku.

Yanga ikiwa imecheza mechi tatu mfululizo bila kupata ushindi itakabiliana na Namungo Fc ikiwa ugenini ikiwa na hasira kali

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.