Yanga imemrejesha Kisinda akitokea klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco
Mkurugenzi wa mashindano wa klabu ya Yanga Saad Kawemba amesema wamemsajili Kisinda kwa ajili ya kumtumia kwenye mashindano ya ndani na michuano ya kimataifa
Taratibu za usajili wake zilikamilika ndani ya dirisha la usajili ikiwa ni pamoja na kupata ITC yake, Yanga ikimbadilisha na Lazarus Kambole kwa ajili ya Ligi ya ndani
Kisinda pia amesajiliwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo awamu ya pili ya dirisha la usajili litafungwa Septemba 15

0 Comments