MWANAMKE AUAWA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA VICHAKANI MKOANI NJOMBE


Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Kifanya kitongoji cha Muungano kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanamke ambaye utambulisho wake haujajulikana anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25-28 aliyekutwa amefariki kwenye shamba la miti

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema hadi sasa mwili wa mwananke huyo umehifadhiwa katika hospitali ya mji Njombe Kibena na kisha kutoa rai kwa wananchi Kwenda kuangalia mwili huo ili uchukuliwe na ndugu.

Katika hatua nyingine Kamanda Issa amewataka wamiliki wa shule binafsi kupeleka mara moja mabasi yanayobeba Watoto kukaguliwa ili kulinda usalama wao wa watoto.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.