MFUASI WA ZUMARIDI AMGEUKA ZUMARIDI MAHAKAMANI, ZUMARIDI AWA MBOGO
MSHTAKIWA namba 17, Hildegard Stanslausi katika kesi ya jinai namba 12 ya mwaka 2022 inayomkabili Mchungaji Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi mkazi wa jijini Mwanza na wenzake 84 amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukiri mahakamani shtaka lake la kushambulia maofisa wa umma na kuwasababishia majeraha.
Stanslausi, baada ya kukiri kosa hilo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Crescensia Mushi aliamua kutumia busara na kuahirisha kesi hiyo kwa saa moja ili kumpa nafasi mshtakiwa kufiria alichokijibu.
Tukio hilo lilitokea leo katika mahakama hiyo baada ya mshitakiwa kusomewa kosa lake na hakimu kumtaka aseme ndiyo kama alifanya ama aseme hapana kama hakufanya, yeye akasema ndiyo, akimaanisha alifanya kosa hilo.
Mshtakiwa huyo alikiri kosa lake na kuiambia mahakama kwamba siku ya tukio akiwa na waumini wenzake walishirikiana kuwaita na kuwachokoza askari na kisha kuanza kuwashambulia.
Baada ya maelezo hayo mahakamani kulizuka sintofahamu baada ya mshtakiwa namba moja, Mchungaji Diana Bundala (Mfalme Zumaridi), kupaza sauti ya juu ndani ya mahakama kumtaka mtuhumiwa huyo kukana kosa.
Imeandikwa na Vitus Audax na Pelusy Yohana (SAUT)
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: