ZA CHINI YA KAPETI....MAJERAHA YA GOTI LA LWANGA SI MCHEZO...DAKTARI SIMBA AKWEPA MTEGO..MKUDE ATAJWA..
SINTOFAHAMU imeibuka ndani ya benchi la ufundi la Simba kuhusiana na hali ya jeraha kwenye goti la kiungo wao nyota, Taddeo Lwanga.
Ingawa bado wahusika Simba hawajataka kufunguka kiundani, lakini vyanzo vya gazeti la Mwanaspoti vimethibisha kuwa majeraha hayo yanaweza kumuweka nje kwa muda mrefu jambo ambalo linaweza kuiathiri Simba ambayo mashabiki wa timu hiyo bado hawaridhishwi na kiwango cha timu yao.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo, Lwanga ameumia goti ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na hilo ni wazi kuwa kiungo mzawa Jonas Mkude amerudi kikosi cha kwanza moja kwa moja .
Chini ya kocha Didier Gomes, Mkude hakuwa na namba katika kikosi cha kwanza na kuna muda hata benchi alikuwa haonekani huku ikielezwa kuwa ni kukosa muda mwingi wa kufanya mazoezi na timu kutokana na sababu mbalimbali lakini tangu aondolewe aliyekuwa kocha mkuu, fundi huyo ameweza kupata nafasi ya kuanzia benchi akipishana na Mzamiru Yassin katika mechi dhidi ya Coastal Union na Namungo FC.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe alipoulizwa kuhusiana na afya za wachezaji hao aligoma kufafanua kwa madai kwamba ameshakabidhi taarifa kwa wakuu wake wa kazi kama taratibu zilivyo.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: