PAMOJA NA YANGA KUFANYA VIZURI..NABI AANIKA KILA KITU WANACHOFANYIWA NA GSM..AUTAJA UONGOZI...

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Jumamosi iliyopita kuichapa Ruvu Shooting juzi bao 3-1, kocha wa Yanga Nasredine Nabi amefunguka kuwa ana ushukuru uongozi wa timu hiyo pamoja na wadhamini wao GSM kwa kufanikisha usajili bora ambao unaendelea kutoa matokeo chanya kila siku

Yanga imefanikiwa kufikisha pointi 15 baada ya kuwachakaza Azam FC na Ruvu katika michezo iliyopigwa klwa nyakati tofauti kwenye Dimba la Mkapa hapa Dar es Salaam.

Nabi alisema kuwa anashukuru uongozi mzima wa Yanga na GSM, kwani walimpatia ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha usajili wa wachezaji aliokuwa anawahitaji.

“ Tunashukuru kwa haya matokeo tuliopata kwani yatatusaidia kuweza kufikia malengo ya timu ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu.

“Nina ushukuru uongozi mzima wa Yanga pamoja na wadhamini wake GSM kwa sapoti yao kubwa walionipatia katika kipindi cha usajili wamesajili wachezaji ambao nilikuwa nawahitaji pia nina imani kuwa tutafikia malengo yetu kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wetu,” alisema kocha huyo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.