TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 06.11.2021: RUDIGER, TER STEGEN, VLAHOVIC, POGBA, BROZOVIC, COMAN, BOWEN

Real Madrid wanatazamia kumsajili mlinzi wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger,28, kwa uhamisho huru baada ya akataba wake na Chelsea utakapokamilika msimu ujao wa joto na wanaweza kumpa mjerumani huyo kitita cha pauni 200,000 kwa wiki. (AS,via Mail)

Mlinda mlango wa Kijerumani anayechezea Barcelona Marc-Andre ter Stegen,29, ni kipaumbele cha usajili wa Newcastle United. (El Nacional)

Maafisa wa Arsenal na Fiorentina walikutana jijini London wiki hii kujadili ofa itakayomfanya mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye miaka 21 kuungana na washika bunduki. (Express)
Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba aliijulisha Manchester United mwaka 2019 kuwa atakuwa tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo mwaka lakini klabu hiyo iliamua vianginevyo. Mkataba wa mchezaji huyo utakamilika majira yajayo ya joto. (Mail)
Kocha mpya wa Tottenham Antonio Conte anataka kumsajili mchezaji wake wa zamani, kiungo wa Inter Milan Marcelo Brozovic. Mchezaji huyo wa miaka 28 ambaye mkataba wake umekwisha msimu wa joto. (Tuttomercato)

Chelsea inataka kumsajili mlinzi wa Hungary anayekipiga Fenerbahce Attila Szalai,23. (Sun)

Barcelona watataka kukatiza mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Uholanzi Luuk de Jong mwenye umri wa miaka 31 kutoka Sevilla mwezi Januari.(Sport -ina Spanish)
Mkufunzi mpya wa Barca Xavi anataka kumfanya winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25, kuwa usajili wake wa kwanza.(Sport-in Spanish)

Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic,23, anashinikiza kuondoka Real Madrid mwezi Januari. (Defensa Central)

Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva,27, alihusishwa na kuondoka Manchester City majira ya joto, lakini amesema ''anafuraha sasa '' ndani ya klabu hiyo. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa West Ham Jarrod Bowen amehusishwa na Liverpool awali na kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp amekiri kuwa anavutiwa na mchezaji huyo mwenye miaka 24. (Liverpool Echo)

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.