SAIDO NTIBANZOKIZA AMVURUGA NABI

BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kucheza mechi yake ya kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ameonekana kuvutiwa na uwezo wake.

Juzi Jumanne, Saido alicheza mechi dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar ambpo aliingia kipindi cha kwanza akitokea benchi kuchukua nafasi ya Yacouba Songne aliyeumia.

Akizungumza na Gazeti la Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema: “Ntibazonkiza alicheza vizuri, ni mchezaji mkubwa na kila mtu anafahamu hilo, ndani ya Yanga kila mtu anayo nafasi ya kucheza kama ambavyo wengine hucheza.“

Siwezi kusema kwa kuhakikisha atacheza katika michezo ijayo, lakini nafasi ni nzuri kwake kutokana na alichokionesha leo (juzi).”

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.