IMEFICHUKA, KUMBE NAMUNGO ILIAHIDIWA MAMILIONI YA FEDHA IKIMFUNGA SIMBA, MAMBO YAWEKWA HADHARANI
SIMBA haitaki mazoea! Unaweza kusema hivyo baada ya jana kuichapa kibishi Namungo bao1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.
Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa kiungo wa Namungo, Abdulaziz Makame akitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu, bao la Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho.
Taarifa za uhakika ,ambazo Soka la Bongo imezinasa kutoka kwa mchezaji mwandamizi wa Namungo ni kuwa walihaidiwa Milioni 30 endapo wangeifunga Simba jana, na milioni 15 endapo wangetoka sare.
"Tulihaidiwa milioni 30 endapo tungepata matokeo ya ushindi au nusu yake kama tungepata sare, ndio maana unaona baada ya mechi wachezaji walijikuta wanyonge sana"
Huo ulikuwa ni mchezo wa tano kwa Simba msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo sasa imefikisha pointi 11 kutokana na kushinda mechi tatu na sare mbili. Bado haijapote ,Msimu uliopita baada ya mechi tano za kwanza, ilikuwa imekusanya pointi 13 baada ya kushinda mechi nne na sare moja.
Kabla ya mchezo wa jana, Simba ilianza msimu kwa suluhu dhidi ya Biashara United, kisha ikaifunga Dodoma Jiji 0-1 ugenini, ikarudi nyumbani kuifunga Polisi Tanzania 1-0, mchezo wa nne dhidi ya Coastal Union, ulimalizika kwa suluhu.
Hivi sasa kikosi hicho kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Hitimana Thiery akisaidiana na Seleman Matola baada ya kuondoshwa kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes.
Ushindi wa jana, umeifanya Simba kupanda hadi nafasi ya pili kutoka ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi 11, ikiachwa pointi nne na vinara, Yanga wenye 15 ambao wameshinda mechi zote tano.Matokeo ya mechi zingine zilizochezwa jana Jumatano ni; Coastal Union 0-0 Prisons na Biashara United 0-0 Mbeya City
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: