REKODI ZA KOCHA MPYA WA SIMBA ZINATISHA, KAMFUNDISHA RONALDO MADRID, KASHINDA LIGI YA MABINGWA ULAYA

KLABU ya Simba SCimeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Pablo Franco Martín (41) raia wa Hispania kukinoa kikosi hicho kuanzia leo Novemba 6, 2021.

Pablo anachukua nafasi ya Didier Gomes Da Rosa raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake ulisitishwa wiki mbili zilizopita baada ya makubaliano ya pande mbili.

Kabla ya kujiunga na Simba alikuwa anafundisha timu ya Al Qadsia SC ya Quwait kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Pablo ni muhumini wa soka la kushambulia alikuwa kocha Msadizi wa Real Madrid mwaka 2018 chini ya Kocha Julen Lopetegui na baadae Santiago Solari ambapo mwaka huo Madrid ilikuwa na wakali kama Cristiano Ronaldo na wengine.

Msimu huo huo, akiwa na Madrid walishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, katika mchezo dhidi ya Livepool .

Mwaka 2015 alikuwa kocha wa Getafe inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania

Years Team
2008–2009 Coria (assistant)

2009–2010 Fuenlabrada (assistant)

2010–2012 Santa Eugenia

2012–2013 Illescas

2013–2014 Puertollano

2014–2015 Getafe B

2015 Getafe

2016 Saburtalo Tbilisi

2017-2018 BSU (assistant)

2018 Real Madrid (assistant)

2019–2021 Al-Qadsia

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.