PAMOJA NA YANGA KUFANYA VIZURI...GSM WASHINDWA KUJIZUA...WALIA KUPATA HASARA..WAITAJA LA LIGA..
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Eng. Hersi Said amesema klabu hiyo inajiendesha kwa hasara.
Eng. Hersi ameyasema hayo jana Novemba 5, 2021 kwenye mahojiano maalum na kipindi cha Kipenga Xtra cha East Africa Radio ambacho huruka Jumatatu hadi Ijumaa saa 6:00 - 7:00 mchana na jana kimeruka kutokea ofisi za GSM.
''Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara'', ameeleza Eng. Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM.
Aidha kuhusu mabadiliko amesema kuwa ''Tumechagua mfumo wa wanachama na wawekezaji kwa 51% kwa wanachama na 49% kwa wawekezaji. Hili tumejifunza La Liga na ndio maana unaweza ukaona kwanini Real Madrid na Barcelona zinapendwa na watu duniani. Tumejifunza kitu kikubwa sana na mabadiliko ya Yanga yatakwenda kuwa ya mfano''.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: